Type Here to Get Search Results !

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI TUME YA UTUMISHI WA BUNGE

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI TUME YA UTUMISHI WA BUNGE


MWAJIRI: PARLIAMENT OF TANZANIA

KADA: AFISA HESABU DARAJA LA II (ACCOUNTS OFFICER II)

TAREHE YA USAILI WA MCHUJO: 27 May 2023

MUDA: 07:00:00 AM

MAHALI: CHUO KIKUU CHA DODOMA - COLLEGE OF EDUCATION (THEATRE 3 & 4)

TAREHE YA USAILI WA MAHOJIANO: 29 May 2023

MUDA: 09:00:00 AM

MAHALI: OFISI ZA BUNGE - DODOMA

Katibu wa Bunge, kwa niaba ya Sekretarieti ya Bunge anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 27 Mei, 2023 hadi 03 Juni, 2023 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

i. Usaili utafanyika kuanzia tarehe 27 Mei, 2023 hadi 03 Juni, 2023 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.

ii. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)

iii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;

iv. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.

v. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI, Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.

vi. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.

vii. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.

viii. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.

ix. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)

x. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.

xi. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.

xii. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya usaili kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili

xiii. Wasailiwa wote mnajulishwa kuwa hali ya hewa ya Jiji la Dodoma ni baridi hivyo mnashauriwa kuvaa nguo zinazohimili hali ya hewa ya ubaridi.

xiv. Msailiwa haruhusiwi kuja na simu au kifaa chochote cha kielekroniki kwenye eneo la usaili.

SOMA HAPA RATIBA YA USAILI NA MAJINA YA WALIOITWA

Post a Comment

0 Comments