Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa aya ya 145 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha kwa mujibu wa tangazo la Serikali Na.11 Vol.95 la tarehe 14 Machi, 2014 ikisomwa pamoja na marekebisho ya Sheria ya Utumishi wa Umma Na.18/2007, Halmashauri mbali ya kuwa na majuku mengine, inalo jukumu la kuajiri watumishi wa kada mbalimbali za Halmashauri.
Hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa anawatangazia Watanzania wenye sifa zilizoainishwa hapa chini na ambao wapo tayari kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kuleta maombi yao ya kazi. Nafasi hizo ni kwa Watanzania wote.
1. MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II - NAFASI 4
Sifa za mwombaji:
- Awe amehitimu na kufaulu kidato cha Nne (IV)
- Awe amehudhuria mafunzo ya Stashahada (DIPLOMA) ya Uhazili na kufaulu mtihani wa hatua ya tatu
- Awe amefaulu somo la Hati Mkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja
- Awe amepata mafunzo ya Kompyuta katika Chuo kinachotambulika na Serikali na kupata Cheti katika Programu za Windows, Microsoft Office, Internet, Email na Publisher.
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA NYASA
Tafadhali hakikisha unatembelea Ajiriwa Serikalini kujua nafasi mpya za kazi zinazotangazwa kila siku kutoka Halmashauri mbalimbali na taasisi zote za Serikali.