Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi anapenda kuwatangazia Wanzania wote wenye sifa zilizoorodheshwa kwenye tangazo hili kujaza nafasi kumi na mbili (12) za ajira ya kudumu ya Mtendaji wa Kijiji Daraja la III na Katibu Mahsusi Daraja la III nafasi nne (4). Ajira hizo zimetokana na kibali cha ajira mpya kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia barua yenye kumb.Na.FA.97/228/9 ya tarehe 13 Mei 2022.
Tafadhali bonyeza kwenye jina la ajira husika kama zilivyoorodheshwa hapo chini ili kusoma maelezo kamili ya nafasi husika kama vile sifa za mwombaji, kazi na majukumu, ngazi ya mshahara pamoja na jinsi ya kutuma maombi.
ZINGATIA: Maombi yatapokelewa kuanzia tarehe 24/05/2022 hadi tarehe 06/06/2022.
1.0: MTENDAJI WA KIJIJI III (VILLAGE EXECUTIVE III) (NAFASI 12)
2.0: KATIBU MAHSUSI III (PERSONAL SECRETARY III) (NAFASI 4)
This comment has been removed by the author.
ReplyDelete