Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo amepokea kibali cha ajira mpya kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Kwa hiyo anawatangazia Watanzania wote wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi kumi (10) za Mtendaji wa Kijiji Daraja la III.
Tafadhali bonyeza kwenye jina la nafasi ya kazi hapo chini ili kusoma maelezo kamili ya ajira hii kama vile sifa za mwombaji, kazi na majukumu, ngazi ya mshahara pamoja na jinsi ya kutuma maombi.
ZINGATIA: Maombi yatumwe kabla ya tarehe 06/06/2022.
1.0: MTENDAJI WA KIJIJI III (VILLAGE EXECUTIVE III)