Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti imepokea kibali cha kutekeleza ikama na Bajeti kwa ajira mpya katika mwaka wa fedha 2021/2022 chenye kumb.Na.FA.97/228/01/9 cha tarehe 13 Mei 2022 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti anawatangazia wananchi wote raia wa Tanzania wenye sifa kuomba nafasi zilizoorodheshwa hapo chini.
Tafadhali bonyeza kwenye jina la ajira husika kama zilivyoorodheshwa hapo chini ili kusoma maelezo kamili ya nafasi husika kama vile sifa za mwombaji, kazi na majukumu, ngazi ya mshahara pamoja na jinsi ya kutuma maombi.
ZINGATIA: Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 06/06/2022 saa 09:30 alasiri.
- MTENDAJI WA KIJIJI III (VILLAGE EXECUTIVE III) (NAFASI 13)
- MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II (RECORDS MANAGEMENT) (NAFASI 5)
- KATIBU MAHSUSI III (PERSONAL SECRETARY III) (NAFASI 3)
- DEREVA DARAJA II (NAFASI 3)