POST: AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA III
POST CATEGORY(S): FARMING AND AGRIBUSINESS
EMPLOYER: Tanzania Agricultural Research Institute (TARI)
APPLICATION DEADLINE: 08 June 2021
JOB SUMMARY: N/A
DUTIES AND RESPONSIBILITIES
i. Kushirikiana na Wakulima kuendesha mashamba ya majaribio na mashamba darasa;
ii. Kutembelea Wakulima/vikundi vya Wakulima katika mashamba yao na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya mbinu bora na za kisasa za kilimo cha kibiashara;
iii. Kufundisha na kuwaeleza Wakulima juu ya matumizi bora ya mbolea, madawa na zana za kilimo;
iv. Kukusanya na kutunza takwimu za hali ya kilimo katika Kijiji;
v. Kubuni na kuandaa vihenge vya kisasa vya hifadhi ya mazao na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mazao;
vi. Kutoa taarifa juu ya dalili za kuwepo visumbufu vya mimea na mazao;
vii. Kuandaa na kutumia daftari la kilimo katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku;
viii. Kushiriki katika mchakato wa kuibua fursa na vikwazo vya maendeleo na kuandaa Mpango wa Maendeleo ya Kilimo wa kijiji; na
ix. Kuandaa taarifa ya utekelezaji ya kila mwezi na kuiwasilisha kwa Afisa Ugani wa kata na nakala kuiwasilisha kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji.
QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne (IV) wenye Astashahada ya Kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
REMUNERATION: TGS B