POST: MKAGUZI WA DARAJA LA II
POST CATEGORY(S): ACCOUNTING AND AUDITING
EMPLOYER: NATIONAL AUDIT OFFICE (NAOT)
APPLICATION DEADLINE: 03 June 2021
DUTIES AND RESPONSIBILITIES
i. Kukagua nyaraka za matumizi, maendeleo, amana, wakala, mifuko, miradi maalum na mapato ya Serikali;
ii. Kushiriki kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mpango wa kazi wa ukaguzi kila mwaka;
iii. Kushiriki kufanya tathmini ya mpango wa kazi na kupendekeza mabadiliko inapobidi kulingana na tathmini ya taarifa ya utekelezaji ya mpango wa kazi;
iv. Kuhakikisha kuwa hoja na barua za ukaguzi zinatolewa na kushughulikiwa kwa wakati unaotakiwa;
V. Kushiriki kutayarisha na kutekeleza mpango wa ukaguzi (Audit Programme;
VI. Kushiriki kupanga na kuratibu mpango wa kazi za ukaguzi;
VII. Kutayarisha hoja na barua za ukaguzi; na
VIII. Kutunza daftari za kumbukumbu mbalimbali za hesabu katika kituo chake kwa maelekezo ya kiongozi mahali pa kazi.
QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Wahitimu wa Shahada ya Biashara/Sanaa yenye mwelekeo wa uhasibu au Stashahada ya juu ya Uhasibu (Advanced Diploma in Accounting) kutoka vyuo au taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali.
REMUNERATION: TGS D