Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) anapenda kuwataarifu Waombaji wote wa kazi zilizotangazwa kupitia tangazo lenye Kumb. Na. CA.434/463/01/104 la tarehe 25 Aprili, 2023, kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 27 Mei 2023 na tarehe 29 Mei, 2023 katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
1. Usaili wa mtihani wa kuandika (written interview) utafanyika tarehe 27 Mei, 2023 kama inavyoonekana kwenye kada husika saa 1:00 kamili asubuhi.
2. Usaili wa mahojiano ya ana kwa ana (Oral Interview) utafanyika tarehe 29 Mei, 2023 kama inavyoonekana kwenye kada husika saa 1:00 kamili asubuhi.
3. Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.
4. Vitambulisho vitakavyokubalika siku ya usaili ni pamoja na:- Kitambulisho cha mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha uraia (NIDA), Hati ya kusafiria au Leseni ya Udereva.
5. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, Kidato cha VI na Shahada kutegemeana na mahitaji ya tangazo la kazi na sifa za Mwombaji.
6. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials; Matokeo ambayo hayajakamilika (Provisional Statement of Results) au hati za matokeo za kidato cha IV na VI (Results Slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
7. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
8. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU, NACTE au NECTA).
Kada zinazohusika ni kama zifuatazo;
- KADA: TUTORIAL ASSISTANT - ACCOUNTING AND FINANCE, MWAJIRI: CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA
- KADA: TUTORIAL ASSISTANT- ENVIRONMENTAL HEALTH SCIENCES, MWAJIRI: CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA
- KADA: TUTORIAL ASSISTANT- MICROBIOLOGY/APPLIED MICROBIOLOGY, MWAJIRI: CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA
- KADA: TUTORIAL ASSISTANT- MULTIMEDIA TECHNOLOGY, MWAJIRI: CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA
- KADA: TUTORIAL ASSISTANT- URBAN PLANNIN/URBAN AND REGIONAL PLANNING, MWAJIRI: CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA
- KADA: TUTORIAL ASSISTANT- CIVIL ENGINEERING, MWAJIRI: CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA
- KADA: TUTORIAL ASSISTANT- ELECTRICAL ENGINEERING, MWAJIRI: CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA
- KADA: TUTORIAL ASSISTANT- BUSINESS ADMINISTRATION (RUKWA CAMPUS COLLEGE, MWAJIRI: CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA
- KADA: ASSISTANT LECTURER - MASS COMMUNICATION, MWAJIRI: CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA
- KADA: ASSISTANT LECTURER – MECHANICAL ENGINEERING, MWAJIRI: CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA
- KADA: ASSISTANT LECTURER- FOOD ENGINEERING, MWAJIRI: CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA
- KADA: ASSISTANT LECTURER- EPIDEMIOLOGY & BIOSTATISTICS, MWAJIRI: CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA
- KADA: ASSISTANT LECTURER- MEDICAL LABORATORY, MWAJIRI: CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA
- KADA: ASSISTANT LECTURER- MINING ENGINEERING, MWAJIRI: CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA
- KADA: ASSISTANT LECTURER- INFORMATION AND COMMUNICATION TECHNOLOGY (RUKWA CAMPUS COLLEGE), MWAJIRI: CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA
- KADA: ASSISTANT LECTURER - DATA SCIENCE, MWAJIRI: CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA
- KADA: ASSISTANT LECTURER - CROP SCIENCE, MWAJIRI: CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA
- KADA: ASSISTANT LECTURER- URBAN PLANNING/URBAN AND REGIONAL PLANNING, MWAJIRI: CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA