JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kum.Na.JA.9/259/01/80
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Bunge la Tanzania anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi moja (1) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.
1.0 MWAJIRI: BUNGE LA TANZANIA
1.0.1 MWANDISHI WA TAARIFA RASMI ZA BUNGE II (NAFASI 1)
1.0.2 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandika majadiliano ya vikao vya Kamati na Bunge yaliyorekeishwa katika sauti;
ii. Kuandika na kuhakiki michango ya maandishi ya Wabunge;
iii. Kufanya uhariri wa awali wa nakala za majadiliano kabla ya kuziwasilisha kwa Wabunge husika;
iv. Kuingiza masahihisho yaliyofanywa na Wabunge katika nakala za awali za Taarifa Rasmi za Bunge;
v. Kuhifadhi nakala tepe za awali za majadiliano ya vikao vya Kamati za Bunge
vi. Kufanya kazi nyingine za kiofisi atakazopangiwa na msimamizi wake wa kazi.
1.0.3 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye Shahada ya kwanza katika fani ya Uhazili kutoka Chuo Kikuu au Taasisi ya Elimu ya Juu inayotambuliwa na Serikali.
1.0.4 MSHAHARA: PSS D
MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na Baraza la Elimu ya Ufundi Tanzania (NACTE).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 18 Mei, 2022.
Muhimu, kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
S.L.P. 2320, CHUO KIKUU CHA DODOMA(UDOM) JENGO LA UTUMISHI/ASHA
ROSE MIGIRO, DODOMA.
i. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
ii. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Limetolewa na;
KATIBU
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA