Type Here to Get Search Results !

Majina ya walioitwa kwenye usaili Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mei 2022

 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Majina ya walioitwa kwenye usaili Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mei 2022


OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA


Imetolewa 10 Mei, 2022.

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 21 Mei 2022 - 28 Mei, 2022 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo: -

i. Usaili utafanyika tarehe 21 Mei 2022 - 28 Mei, 2022 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada;

ii. Usaili wa Mchujo (kuandika) kwa kada za Mamlaka ya Bandari Tanzania utafanyika tarehe 21 Mei, 2022, Usaili wa Vitendo 23 Mei, 2022 mpaka tarehe 27 Mei, 2022 na usaili wa Mahojiano ya ana kwa ana utafanyika tarehe 26, Mei, 2022 mpaka tarehe 28 Mei, 2022.

iii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;

iv. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria;

v. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;

vi. Wasailiwa watakaowasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;

vii. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;

viii. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;

ix. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA);

x. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.

xi. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.

xii. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.

xiii. Wasailiwa wanatakiwa kuvaa barakoa muda wote wanapokuwa kwenye maeneo ya Usaili.

CLICK HAPA | RATIBA YA USAILI NA MAJINA YA WASAILIWA

Post a Comment

0 Comments