Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Newala anapenda kuwatangazia Watanzania wote wenye sifa kutuma maombi kwa kazi ifuatayo:-
Mtendaji wa Mtaa Daraja la III - (NAFASI 14)
Sifa za Kitaaluma kwa mwombaji
- Awe amefaulu Kidato cha nne (IV) au sita (VI)
- Awe amefaulu mafunzo ya Astashahada (Cheti) "NTA Level 5" katika fani zifuatazo:- Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii au Sayansi ya jamii kutoka Chuo chochote kinachotambulika Serikali.
Kazi na Majukumu ya Mtendaji wa Mtaa
- Kuwa Katibu wa Kamati ya Mtaa
- Mtendaji Mkuu wa Mtaa
- Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zilizotekelezwa na Halmashauri katika Mtaa
- Kuwajibika kwa Mtendaji wa Kata
MSHAHARA
Cheo cha Mtendaji wa Mtaa daraja la III kina mshahara wa TGS B kwa Mwezi
MASHARTI YA JUMLA
- Mwombaji awe Mtanzania mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45
- Mwombaji aambatanishe cheti cha kuzaliwa
- Mwombaji ambaye ni mtumishi wa Umma apitishe barua yake ya maombi kwa mwajiri wake
- Mwombaji aambatanishe maelezo yake binafsi yanayojitosheleza (CV) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa kuaminika pamoja na namba zao za simu.
- Maombi yote yaambatanishwe na nakala za vyeti vya elimu na taaluma kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali
- Testimonials, Provisional results, Statements of results n.k hazikubaliki
- Waombaji waweke picha pamoja na passport size katika barua zao za maombi
- Waombaji wote ambao wamesoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vinafanyiwa ulinganishi na TCU na NACTE
- Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 03/06/2022 saa tisa alasiri
Barua zote zitumwe kwa anuani iliyopo hapa chini
MKURUGENZI WA MJI,
HALMASHAURI YA MJI NEWALA,
186 BARABARA YA MASASI,
MTAA WA TUPENDANE,
S.L.P 39,
63482 NEWALA.
