TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Kufuatia kutolewa kwa Tangazo lenye Kumb.Na.KTC/L50/22/07 la tarehe 27/04/2021 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa anawatangazia wafuatao kufika kwenye Usaili utakaofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 08-09/06/2021 Katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kondoa (Jengo Jipya) kuanzia saa 03:00 kamili asubuhi.
Ni muhimu kuja na vitu vifuatavyo: -
- Vyeti halisi vya Elimu (Original)
- Vyeti halisi vya Taaluma (Original)
- Kitambulisho cha Taifa, kura, mkazi, hati ya kusafiria (kimoja wapo)
- Cheti halisi cha kuzaliwa
- Picha moja (1) (passport size) yenye kitambaa cha bluu nyuma
- Barakoa kwa ajili ya kujikinga na Virusi vya Corona
NB: Gharama zote za usaili zitakuwa kwa msailiwa (Nauli, Malazi, Chakula na Kalamu). Ambaye hatafika na vitu hivyo hataweza kushiriki katika usaili.
Kuona orodha kamili ya majina ya watu walioitwa kwenye usaili soma kwenye; ORODHA YA WALIOITWA KWENYE USAILI