Type Here to Get Search Results !

TANGAZO KWA WAOMBAJI KAZI WA NAFASI YA “TAX INVESTIGATION OFFICER II” TRA

TANGAZO KWA WAOMBAJI KAZI WA NAFASI YA “TAX INVESTIGATION OFFICER II” ILIYOTANGAZWA KWA NIABA YA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA) TAREHE 01 JUNI, 2021


Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwajulisha waombaji kazi wote wa nafasi ya “TAX INVESTIGATION OFFICER II” iliyotangazwa tarehe 1 Juni, 2021 kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwa nafasi hiyo imefutwa. Hivyo maombi ya nafasi hiyo hayatoendelea kupokelewa kutokana na sababu zilizoelekezwa na Mwajiri. Aidha, nafasi hizo 2 zilizofutwa zimeongezwa kwenye kada ya “TAX MANAGEMENT OFFICER II” kutoka nafasi 22 zilizotangazwa awali na kuwa 24 kwa sasa.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza baada ya kutoa taarifa hii.

Kwa huduma mbalimbali au ufafanuzi tafadhali wasiliana nasi kupitia simu za kiganjani ambazo ni 0736-005511, 0735-398259 au 0784-398259.

Tangazo hili limetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

02 Juni, 2021.

Post a Comment

0 Comments