Hili ni tangazo la kuitwa kwenye usaili Taasisi mbalimbali za Serikali lililotolewa na Sekretarieti ya Ajira (PSRS) tarehe 18 June 2021.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Institute of Adult Education (IAE), Taasisi ya Sanaa Bagamoyo (TASUBA), Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA), Tanzania Food and Nutrition Centre (TFNC), Tanzania Railways Corporation (TRC), The Land Transport Regulatory Authority (LATRA), Muhimbili National Hospital (MNH), Tanzania Agricultural Research Institute (TARI), Wizara ya Mifugo na Uvuvi, National Audit Office (NAOT), Tabora Urban Water Supply and Sewerage Authority (TUWASA), Arusha Technical College (ATC), Wizara ya Fedha na Mipango (MOF), Halmashauri ya Wilaya Pangani, Halmashauri ya Wilaya Meru, Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, Katibu Tawala wa Mikoa Shinyanga, Tengeru Institute of Community Develoment (TICD), TanzaniaInsurance Regulatory Authority (TIRA) na Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 26 Juni, 2021 hadi 30Juni, 2021 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i. Usaili utafanyika kuanzia tarehe 26 Juni hadi 30 Juni, 2021 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada;
ii. Kila Msailiwa anapaswa kunukuu kwa usahihi namba yake ya usaili wa mchujo na Vitendo, namba hizo zinapatikana kwenye akaunti ya kila Msailiwa katika mfumo wa maombi ya kazi;
iii. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa;
iv. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
v. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria;
vi. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
vii. Wasailiwa watakaowasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
viii. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi;
ix. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
x. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA);
xi. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
xii. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
xiii. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.
Kujua kuhusu ratiba ya usaili na majina ya wasailiwa tafadhali fungua kiambatanisho hapo chini;
MAELEZO KAMILI YA TANGAZO | CLICK HERE