Nafasi ya kazi: MKUFUNZI II (DAKTARI WA MIFUGO), Zipo nafasi 4
EMPLOYER: Livestock Training Agency (LITA)
APPLICATION TIMELINE: 2021-06-08 2021-06-21
DUTIES AND RESPONSIBILITIES
i.Kutafsiri mitaala na kufundisha ngazi ya NTA Level 4-6,
ii.Kutunga na kusimamia Mitihani ya upimaji na na mitihani ya mwisho wa muhula,
iii.Kuandaa “Training materials” na learning resources” na kuwapatia wanafunzi,
iv.Kuwasimamia na kuwasaidia wakufunzi wasaidizi,
v.Kusimamia mafunzo kwa vitendo vyuoni na uwandani,
vi.Kutambua mahitaji ya wanafunzi wenye uhitaji maalum na kuwasaidia,
vii.Kutoa mafunzo na ushauri kwa wafugaji na wadau wengine katika sekta ya mifugo,
viii.Kuandaa na kusimamia midahalo ya masomo ya wanafunzi,
ix.Kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wadau wengine na;
x.Kufanya kazi zingine zitakazotolewa na viongozi.
QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Awe amehitimu shahada ya kwanza ya Sayansi ya Tiba ya Mifugo kutoka chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali na kusajiliwa na Baraza la Veterinari Tanzania (VTC). Awe amefaulu kwa angalau wastani wa alama B katika masomo yake yote.
REMUNERATION: PTSS 11