Halmashauri ya Wilaya ya Musoma inahitaji mtu wa kujaza nafasi wazi ya ajira ya Msaidizi wa Hesabu ( Accounts Assistant) mwenye uwezo wa kufanya amajukumu yafuatayo;
- Kuandika na kutunza “register” zinazohusu shughuli za uhasibu;
- Kutunza Kumbukumbu za hesabu;
- Kupeleka barua/nyaraka za uhasibu Benki; na
- Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
SIFA NA UZOEFU VINAVYOHITAJIKA;
Uwe na Cheti cha Astashahada ya Uhasibu kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali au Cheti cha ATEC I kinachotolewa na NBAA au sifa zingine zinazolingana na hizo zinazotambulika na NBAA.
NGAZI YA MSHAHARA: TGS B