Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi kama ifuatavyo;-
1.0 MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III – NAFASI 5.
1.1 SIFA ZA MWOMBAJI:-
1. Awe na Elimu ya Kidato cha Nne/ Sita
2. Awe amehitimu mafunzo ya Astashahada/ Cheti NTA LEVEL 5 katika moja ya fani zifuatazo.
Utawala
Rasilimali watu
Sheria
Maendeleo ya Jamii
Elimu ya Jamii
Usimamizi wa fedha au
Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali
3. Awe na Umri usiopungua miaka kumi na nane (18) na usiozidi Miaka arobaini na tano (45)
4. Awe amesajiliwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) mwenye kadi au namba ya usajili wa NIDA
1.2 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Viwango vya Serikali kwa ngazi ya Mshahara TGS B kwa mwezi
1.3 MAJUKUMU YA KAZI
Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.
Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji
Kuratibu Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
Kutafsiri na Kusimamia Sera, Sheria na taratibu za uendeshaji wa Serikali ya Kijiji
Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha
wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali
Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji
1.4 MASHARTI YA JUMLA
Awe Raia wa Tanzania
“Testimonials Provisional Results, Statement of Result” na hati za matokeo kidato cha Nne na Sita (Form IV na VI na Result Slips) HAVITAKUBALIWA
Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimekaguliwa na kuthibitishwa na mamlaka husika (NECTA, NACTE NA TCU)
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
1.5 NAMNA YA KUTUMA MAOMBI;-
Kila muombaji wa kazi awasilishe barua ikiambatishwa na;-
Wasifu Binafsi (CV)
Vivuli vya Vyeti Elimu na Ujuzi
Cheti cha Kuzaliwa
Picha mbili za “Passport Size”
1.6 Maombi yote yatumwe kupitia anuani ya posta kama ifuatavyo;-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 263,
IFAKARA
1.7 Mwisho wa kupokea Maombi ni tarehe 26/07/2021 siku ya Jumatatu ,saa 9.30 alasiri.
Imetolewa na:
Eng. Stephano B. Kaliwa,
MKURUGENZI MTENDAJI (W),
MLIMBA.
Source: Ajira.go.tz