TANGAZO LA NAFASI ZAKAZI
1. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Msalala kupitia kibali cha ajira mbadala chenye Kumb.Na.FA.170l376rc1f8"146 cha tarehe 06 April, 2021 kilichotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishiwa Umma na Utawala Bora, anatangaza nafasi zakazi kwa wananchi wa Tanzaniawenye sifa na ujuzi wa kujaza nafasi zifuatazo:-
2. MTENDAJT WA KIJlJl III - NAFASI MOJA (1)
2.1 Sifa za Muombaji,
Awe na elimuya kidato cha Nne (lV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani za Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au chuo chochote kinachotambulika na serikali
2.2. Ngazi ya Mshahara
TGS. B, kwa kuzingatia viwango vya Serikali
2.3. Majukumu ya Kazi
l. Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
ll. Kusimamia Ulinzi na Utawala Bora kwa Raia na mali zao. Kuwa mlinzi wa amani na msirnamiziwa Utawala bora katika Kijiji.
lll. Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo katika Kijiji
lV. Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
V. Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
VI. Kuandaa taarifa za utekelezali wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini na kuongeza uzalishaji mali.
Vll. Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji
Vlll. Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbuu zote na nyaraka za Kijiji
lX. Kuwa mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika Kijiji
X. Kupokea,kusikiliza na kutatua migogoro ya wananchi
Xl. Kusimamia utungajiwa Sheria ndogo zaKijiji na
Xll. Atawajibika kwa Mtendajiwa Kata
3. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II - NAFAST MOJA (1)
3.1. Sifa za Muombaji,
Awe amehitimu kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) na mwenye cheti cha utunzaji kumbukumbu katika mojawapo ya fani za Afya, Masjala, Mahakama na Ardhi.
3.2. Ngazi ya Mshahara,
TGS.B Kwa kuzingatia viwango vya serikali
3.3. Majukumu ya Kazi,
l. Kutafuta kumbukumbu/nyarakalmafaili yanayohitajika na wasomaji
Il. Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka
lll. Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (Classification of boxing) kwaajili ya matumizi ya Ofisi
lV. Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki ( file racks/cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu
V. Kuweka kumbukumbu (barua,nyaraka n.k.) katika mafaili
V. Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/ nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.
4. MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE
I. Waombajiwote wawe Raia wa Tanzania wanye umri usiozidi miaka 45
ll. Waombaji waambatanishe cheti cha kuzaliwa
Ill. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referebs) wa kuaminika
IV. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo na vyeti vya kidato cha Nne na Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
V. Testimonials, "Provision Resu/b'i "statements of Results", hati ya matokeo ya kidato cha Nne na Sita HAVITAKUBALIWA
VI. Waombaji waambatishe picha moja "Pasport Size" ya hivi karibuni
VII. Mwisho wa kutuma maombi nitarehe 1310512021
NB; Tangazo hili linapatikana katika tovuti ya Halmashauri ded@msalaladc.go.tz, tovuti ya secretarieti ya ajira www.ajira.go.tz na katika mbao za matangazo za Halmashauri.
Maombi yote yatumwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashaui ya Wilaya Msalala
S.L.P 16
KAHAMA